nitajiuzulu Siasa.”
Ifikapo mwaka 2015, CCM itakuwa imetawala
Tanzania kwa miaka 54 mfululizo. Kwa
Mtanzania aliyeajiriwa, huu ni umri wa kustaafu
na kujipanga kula pensheni. Umri huu pia
unalingana na wastani wa maisha ya mtanzania
(life expectancy). Kwa kila hali, miaka 54 ni
miaka mingi sana. Katika mazingira ya kisiasa,
jambo hili sio rahisi kutokea katika nchi yoyote
ile inayofuata mfumo wa vyama vingi, hasa
katika nyakati hizi za demokrasia ya kiliberali
(liberal democracy), soko huria (free market) na
utawandawazi (globalization).
Utawala wa CCM kwa miaka zaidi ya hamsini
(50) umeambatana na uwepo wa ‘amani’ na
‘utulivu’, suala ambalo ni moja ya mafanikiio
makubwa ya kisiasa kwa CCM. Lakini ni vizuri
tukaambiana ukweli – hatuna utulivu Tanzania
bali uvumilivu. Vinginevyo kama alivyotamka
Nyerere mwaka 1987, ipo siku bomu litalipuka
kwani kufaulu kwa CCM kisiasa kunaenda
sambamba na kufeli katika nyanja za kiuchumi na
kijamii. Kwa mfano, pamoja na kuishi katika
mazingira ya amani na utulivu, Mwanakijiji wa
Tanzania amekuwa mvumilivu sana kusuburi
pengine ipo siku ahadi za TANU wakati wa
harakati za uhuru zitatimizwa. Vinginevyo,
maisha ya mwanakijiji leo sio tofauti sana na
yale ya 50 iliyopita. Isitoshe, tofauti na enzi za
Ujamaa, leo wageni wale wale tuliowafukuza
kutokana na kuiba rasilimali zetu wanapokewa
kwa mikono miwili; wizi wa fedha za walipa kodi
ni umeongezeka; matumizi ya rasilimali za nchi
yanafaidisha wachache zaidi; tofauti ya kipato
baina ya walio nacho na wasio nacho imekuwa
kubwa zaidi; dira na mwelekeo kama taifa havipo
tena; na hakuna dalili zozote kwamba hali hii
inaweza kubadilika katika muda mfupi na wa kati
ujao. Ndio maana hata viongozi wengi wa CCM
wanakiri chini kwa chini kwamba ‘The Country is
Suffering From CCM Fatigue’. Huu ndio msingi
wa kauli ya Freeman Mbowe!
Kuna tofauti kubwa baina ya “Doing the Right
Things” na “Doing things Right”, na ili ufanikiwe,
nilazima kufanya yote mawili. Chadema has been
doing the right things ambayo ni kutumia
kikamilifu mapungufu ya CCM kujijenga kisiasa.
Lakini tatizo linakuja kwenye “doing things right”
– ambapo, mbali na kutumia mapungufu ya CCM,
kuna umuhimu wa kufanyia kazi viambato
(ingredients) vinavyoiwezesha CCM kuwa na
mafanikio ya kisiasa. Ushindi wa Chadema
utatokana na umahiri wake kufanyia kazi mambo
kuu tisa kama ifuatavyo:
1. CCM ndio iliyoongoza mageuzi ya kiuchumi
(political reforms) Tanzania;
2. Umiliki na Udhibiti wa Vyombo Vya habari;
3. Uchumi Mkubwa Wa CCM;
4. Ujamaa Bado ni Relevant (unaendana) na
Maisha ya Wengi Vijijini;
5. CCM imejenga Coalition na Taasisi zote nchini
zenye nguvu kiuchumi, kijamii na kijeshi;
6. Katiba ya Sasa ya nchi inaipa CCM nguvu
kubwa kisiasa;
7. Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema
Hazipo Consistent na Coherent;
8. Tanzania inakabiliwa na Udhaifu mkubwa wa
Civil Society; na
9. Political Culture ya Tanzania ina matatizo.
1. Uongozi wa Mageuzi ya Kisiasa
Tume ya Nyalali ilikusanya maoni yaliyoonyesha
kwamba watanzania wengi walipendelea nchi
iendelee na mfumo wa chama kimoja. Lakini
CCM ikaamua kuruhusu maoni ya wachache ndio
yatawale. Ni dhahiri kwamba suala la vyama vingi
lilikuwa haliepukiki lakini mkakati wa CCM wa
kuhakikisha mageuzi ya kisiasa hayatokani na
nguvu ya umma bali CCM na serikali yake
imekijenga sana chama hasa vijijini kwani
nimetembea maeneo mengi na kushangazwa na
maoni ya wengi kwamba wanachofanya chadema
ni “shukrani ya punda ni mateke”. Katika nchi
nyingi maskini, chaguzi kuu zilifanyika muda
mfupi baada ya umma kufanikisha kuleta
demokrasia ya vyama vingi, hivyo kupelekea
vyama vingi tawala kuanguka na kupotea katika
medani za siasa. Nchini Tanzania, mbali ya
kuruhusu vyama vingi kinyume na matakwa ya
wengi, CCM pia ilijiwekea muda wa kutosha
(miaka mitatu) kujiandaa kabla ya kuitisha
uchaguzi wa vyama vingi. Hili ni jambo la kwanza
la Chadema kulifanyia kazi.
2. Umiliki na Udhibiti wa Vyombo Vya Habari
Sina haja ya kujadili hili sana kwani lipo wazi,
lakini muhimu hapa ni mambo mawili: kwanza ni
ile sheria ya mwaka 1976 ambayo hadi leo bado
inatumia na madhara yake yapo wazi; pili, ni
kwamba muundo na utaratibu wa ufanyaji kazi
wa Wizara ya Habari haujabadilika sana na ule
enzi ya kimoja. Wizara hii kwa kiasi fulani bado
ni extension ya idara ya propaganda na uenezi
ya CCM. Chadema ina waziri kivuli wa Habari
ambae he/she is supposed to do “things right” in
that regard.
3. Uchumi Mkubwa wa CCM
Hili lipo wazi kwa Chadema, kwa mfano, katika
ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2000, chadema
iliazimia kurudisha mali zote za CCM serikalini
kwa hoja kwamba mali hizi ziligharimiwa na
watanzania wote chini ya mfumo wa chama
kimoja. Iwapo hoja hii ina mashiko kisheria, basi
kosa linakuja pale Chadema inapoliweka hili
kama ahadi nyakati za uchaguzi badala ya
kulishughulikia kama chama cha upinzani.
Isitoshe, tofauti hii ya kiuchumi baina yake na
CCM inachangia sana Chadema kutofanikisha
malengo yake za kisiasa. Kupitia rasilimali hizi,
CCM pia inafaidika sana na ‘political branding’ .
Siasa ni bidhaa kama nyingine sokoni, kwahiyo
wananchi wanapoona au kusikia ‘brands’ kwa
mfano ‘CCM kirumba’, au maeneo kuitwa “CCM
Makao” etc, brand awareness kupitia macho,
masikio na memory, haina utofauti mkubwa na ile
ya bidhaa nyingine sokonikama Vodacom, CRDB
n.k. Isitoshe, kuna watanzania wengi ambao
wanaamini kwamba Chadema haistahili kuongoza
nchi kwa sababu bado haina fedha. Hii ni imani
potofu na ni muhimu kwa chadema kuanza kutoa
elimu kwa umma kwamba chama chochote cha
siasa kikipewa ridhaa na umma kuongoza nchi,
uwezo wake kufanikisha malengo ya kuendeleza
taifa unatokana na fedha za walipa kodi na
kwamba hivyo ndivyo CCM imekuwa ikifanikiwa
kutawala.
4. Ujamaa Bado ni Relevant (unaendana) na
Maisha ya Wengi Vijijini
Itikadi ya Ujamaa imebakia kuwa nadharia, kwani
kivitendo, CCM inatekeleza sera za soko huria
zinazoendekeza ubepari na elements zote
zinazoendana na mfumo huo. Lakini pamoja na
hayo, bado Ujamaa unaendana na maisha ya asili
aliyokuta mkoloni vijijini. Ndio maana TANU
ilipata wafuasi wengi walioamini kwamba lengo
kuu la TANU ni kumuondoa mkoloni na
kuwarudishia wananchi utamaduni na maisha yao
ya awali. Hali hii pia ilichangia sana Nyerere
kuamua kufuata sera ya Ujamaa mwaka 1967
kwani Tanganyika huru ilikuwa dominated zaidi
na vijiji vilivyosheheni wakulima wadogo wadogo
waliokuwa wanaishi katika umaskini uliopindukia.
Mazingira haya provided “excellent material and
social basis for Ujamaa to flourish” – kwani
dhana ya Ujamaa iliakisi maisha halisi ya walio
wengi; lakini pia malengo ya sera ya Ujamaa na
kujitegemea yaliendana na ndoto za wananchi
wengi.
Tatizo lililopo sasa ni kwamba - Chadema
haijafanikiwa kuja na itikadi ambayo wananchi
wengi (wale waliounga mkono TANU) wanaweza
kuikubali kama ndio mbadala wa kweli wa sera
ya Ujamaa. Ni muhimu kwa Chadema kujipanga
mapema na kurekebisha itikadi yake ya sasa ili
iendane na uhalisia wa maisha ya watanzania
walio wengi, lakini muhimu zaidi, iendane na
ndoto ya watanzania hawa kwani kwa ujumla,
hali zao na ndoto zao hazipishani sana na zile za
enzi ya TANU na uhuru (1950s-1960s), na
uliberali kama sera na itikadi, ambayo hata
Chadema inaifuata, na pia CCM kuitekeleza kwa
miaka zaidi ya 20 sasa, ni chanzo kikubwa cha
umaskini Tanzania.
5. CCM imejenga Coalition na Taasisi zote
nchini zenye nguvu kiuchumi, kijamii na kijeshi.
Kwa mfano, sekta binafsi (wafanyabiashara);
majeshi ya ulinzi na usalama; vyama vya
ushirika; watumishi wa umma; mashirika ya
umma n.k. Tukianza na sekta binafsi, sekta hii ni
muhimu sana katika kusaidia Maendeleo ya
vyama vya siasa na sio kwa Tanzania tu, bali
hata mataifa makubwa. Ingawa sekta hii
haikupewa nafasi wakati wa mfumo wa chama
kimoja, Tanzania huru ilikuwa na tabaka hili
ambalo liliwezeshwa na mfumo wa kikoloni, hasa
wahindi. Sasa ili waendelee na shughuli zao
katika mazingira ya Ujamaa, wengi wao
walitegemea kulindwa na baadhi ya viongozi wa
TANU/CCM, ambao kwa kumzunguka Nyerere,
walianza kuwa washirika wakubwa wa
wafanyabiashara, hasa katika wizi wa rasilimali
za umma. Mfumo wa vyama vingi ulipoingia
mwaka 1992, na pia sekta binafsi kuhalalishwa,
sehemu kubwa ya wafanyabiashara hawa ilikuwa
tayari loyal kwa CCM, hivyo ikawa vigumu kwa
vyama vipya vya siasa kujenga mahusiano na
kada hii.
Kumekuwa na kelele nyingi kwamba CCM
imenunuliwa na wafanyabishara, lakini lazima
tukubaliane kwamba hakuna chama cha siasa
kinachoweza kufanikiwa bila kuwa na uhusiano
wa karibu na wafanyabiashara. Hata Chadema
ikipata mwanya huo, ni muhimu ifanye hivyo, ili
mradi iwe katika mazingira transparent, incorrupt
na yanayozingatia taratibu zilizopo. Isitoshe, ni
sahihi nikisema kwamba bila ya Chadema kuwa
na viongozi kadhaa wenye uwezo mkubwa wa
kifedha, isingefanikiwa kufika ilipo leo.
CCM pia ilishajijenga kwenye vyombo vya ulinzi
na Usalama, kwa mfano, ilikuwa ni kawaida kwa
viongozi wa juu wa jeshi kuwa wajumbe wa
halmashauri kuu ya taifa (NEC) na Kamati Kuu
(CC); vyombo ambavyo hadi leo vina maamuzi ya
juu katika nchi yetu. Nafasi hizi pia walipewa
viongozi wa taasisi za umma (mfano NBC, NIC/
Bima); viongozi wa vyama vya wafanyakazi;
viongozi wa vyama vya ushirika n.k; Pamoja na
mabadiliko ya kutenganisha siasa na utumishi wa
umma, majeshi ya ulinzi na usalama n.k, CCM
bado ina mkono mrefu katika taasisi hizi, hasa
kupitia mamlaka ya uteuzi ya Rais.
6. Katiba ya Sasa ya nchi inaipa CCM nguvu
kubwa kisiasa
Jambo hili tayari linaeleweka lakini nitalijadili
kidogo. Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977
msukumo wake mkubwa ulikuwa ni muungano wa
CCM na ASP (1977), kwani kabla ya muungano
wa vyama hivi viwili, Tanzania haikuwa na katiba
rasmi bali ya mpito kwa miaka karibia kumi tatu:
1964 – 1977. Katiba ya Tanzania (1977)
ilitungwa ili kuhalalisha ufalme wa CCM. Moja ya
mambo muhimu yanayopiganiwa katika
michakato ya katiba mpya katika nchi yoyote ni
“Democracy/democratization of the the society.”
Maana rahisi ya democratization ni - mabadiliko
ya sheria/kanuni/taratibu za msingi za kuongoza
mwenendo na utawala wa nchi husika. Katika
mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya
Tanzania, ni muhimu chadema ikaelewa mambo
mawili:
i. Kwanza ni kukumbushana tu kwani tayari
linajulikana: there has to be a compromise baina
ya nini CCM inataka kiwepo/kisiwepo ndani ya
katiba mpya na nini Chadema pamoja na wadau
wengine wa demokrasia wanataka kiwepo/
kisiwepo ndani ya katiba mpya. Ni vigumu
kushawishika kwamba Chadema (na upinzani kwa
ujumla) itafaidika na mchakato huu kuliko CCM,
hasa ikizingatiwa kwamba uteuzi wa wajumbe wa
tume husika kwa kiasi kikubwa una mkono mrefu
wa CCM. Pia ni vigumu kuelewa kwanini
mwanazuoni incorrupt and sober katika masuala
ya sheria ya katiba, Professor Issa Shivji ambae
anaheshimika kimataifa katika fani hiyo,
hakuteuliwa kwenye tume ya Warioba.
ii. Pili, pamoja na Chadema kufanikiwa kuwa
sehemu ya historia ya katiba mpya, wasijisahau
na kudhania kazi ndio imekwisha kwani kazi ndio
kwanza imeanza. Siasa za katiba mpya
zitatawala sana uchaguzi wa 2015, hasa suala la
muungano. Mwisho wa
karibu kwenye blog inayo husu stori mbali mbali zinazo maisha halisi
Maoni
Chapisha Maoni