nitajiuzulu Siasa.” Ifikapo mwaka 2015, CCM itakuwa imetawala Tanzania kwa miaka 54 mfululizo. Kwa Mtanzania aliyeajiriwa, huu ni umri wa kustaafu na kujipanga kula pensheni. Umri huu pia unalingana na wastani wa maisha ya mtanzania (life expectancy). Kwa kila hali, miaka 54 ni miaka mingi sana. Katika mazingira ya kisiasa, jambo hili sio rahisi kutokea katika nchi yoyote ile inayofuata mfumo wa vyama vingi, hasa katika nyakati hizi za demokrasia ya kiliberali (liberal democracy), soko huria (free market) na utawandawazi (globalization). Utawala wa CCM kwa miaka zaidi ya hamsini (50) umeambatana na uwepo wa ‘amani’ na ‘utulivu’, suala ambalo ni moja ya mafanikiio makubwa ya kisiasa kwa CCM. Lakini ni vizuri tukaambiana ukweli – hatuna utulivu Tanzania bali uvumilivu. Vinginevyo kama alivyotamka Nyerere mwaka 1987, ipo siku bomu litalipuka kwani kufaulu kwa CCM kisiasa kunaenda sambamba na kufeli katika nyanja za kiuchumi na kijam...